MSUVA AWAPIGA BAO MUZAMIRU, KICHUYA NA KUTWAA TUZO YA MCHEZAJI BORA WA VPL MWEZI OKOTOBA
Winga Simon Msuva wa Young Africans amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwezi Oktoba wa Ligi Kuu ya Vodacom.
Msuva
alikuwa na washindani wa karibu wawili katika kinyang'anyiro hicho cha
Oktoba ambao wote ni kutoka Simba. Wachezaji hao ni Shiza Kichuya na
Mzamiru Yassin.
Katika
mwezi Oktoba ambao ulikuwa na raundi sita, Msuva aliisaidia timu yake
kupata jumla ya pointi 14 huku akifunga mabao manne, na kutoa pasi tano
za mwisho (assist).
Kwa
kushinda tuzo ya mchezaji bora wa mwezi, Msuva ambaye alikuwa mchezaji
bora wa Ligi Kuu ya Vodacom kwa msimu wa 2014/2015 atazawadiwa kitita
cha sh. milioni moja kutoka kwa wadhamini wa Ligi hiyo kampuni ya
Vodacom Tanzania.