Mbowe: Majaliwa afukuzwe kazi kwa ‘rushwa’


Kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni, Freeman Mbowe amemtaka rais John Magufuli kumfukuza kazi waziri mkuu, Kassim Majaliwa kwa madai kuwa ameshiriki kupanga mpango wa siri wa kuwapa rushwa ya 10m/- wabunge wa CCM ili kuwezesha uungwaji mkono na upitishwaji wa Muswada wa Huduma za Habari wa mwaka 2016.

Akizungumza kwenye kipindi cha maswali  na majibu kwa waziri mkuu bungeni, Mbowe alidai kuwa Jumanne iliyopita waziri mkuu alifanya kikao na katibu mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na wabunge wa chama hicho kujadili pendekezo la mpango wa maendeleo Muswada wa Huduma za Habari.
Kwa mujibu wa mbunge huyo wa Hai, kikao hicho kilikubaliana kila mbunge wa CCM apewe 10m/- ili kuwalainisha waweze kupitishwa muswada huo na mpango wa serikali wa maendeleo.

‘Mheshimiwa waziri mkuu, liambie bunge hili iwapo madai haya ni kweli au ni uongo’ Alisema Mbowe.

Hata hivyo naibu spika aliingilia na kudai swali hilo sio la kisera.

Baada ya vipindi vha bunge kumalizika Mbowe aliitisha mkutano na waandishi wa habari na kufafanua madai yake na kusema rushwa hiyo imevunja rekodi kwakuwa wabunge wote wa CCM 260 walipewa rushwa.
Naye mnadhimu mkuu wa kambi ya upinzani, Tundu Lissu alisema kuwa rushwa hiyo ni kipimo madhubuti kwa rais Magufuli hususani kwenye mapambano dhidi ya ubadhirifu.
Powered by Blogger.