Wilaya ya Kongwa yazindua Kampeni ya Kupambana na Baa la Njaa
Mkuu wa wilaya ya Kongwa Mh Deo Ndejembi akizungumza mara baada ya kuzindua kampeni ya kuondoa Njaa wilaya ya Kongwa, (ONJAKO).
Mkuu wa wilaya ya Kongwa Mh Deo Ndejembi akizindua kampeni ya kuondoa Njaa wilaya ya Kongwa, (ONJAKO).
Ofisa Kilimo Mkoa wa Dodoma Bi Aziza Mumba akisisitiza jambo wakati wa uzinduzi wa Okoa Njaa Wilayani Kongwa.
Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa Richard Mwite.
Mkuu
wa Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma Mhe Deo Ndejembi akisisitiza vijana
Kulima na kuacha kucheza mchezo wa Pool Table wakati wa kazi.
Mkuu
wa Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma Mhe Deo Ndejembi ameanzisha kampeni ya
kuondoa Njaa wilaya ya Kongwa, (ONJAKO) yenye dhamira ya kuwasaidia
wananchi kuondokana na hali yanjaa ambayo ni kadhia kubwa katika maeneo
mbalimbali ya Wilaya hiyo sambamba na Taifa kwa ujumla.
Kuanzishwa
kwa Kampeni ya Okoa njaa Wilaya ya Kongwa imejili wakati Mkuu huyo wa
Wilaya ya Kongwa Akizungumza na Wakuuwa Idara na vitengo, Madiwani wa
Kata zote zilizopo Wilayani humo, Watendaji wa Kata, Maafisa Tarafa,
Waratibu Elimu Kata, Wenyeviti wa Vijiji vyote 87 vya Wilaya ya Kongwa
na watendaji wao, pamoja na wadau waalikwa na Kilimo.
Akizindua
kampeni hiyo Dc Ndejembi alisema kuwa Kampeni hiyo imezinduliwa Mwezi
Octoba kwa ajili ya msimu wa mwaka 2016/2017 na inatarajiwa kuwa kampeni
Endelevu katika kipindi cha Miaka mitano.
Ameeleza
kuwa huu ni mkakati maalumu katika Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma ili
kukabiliana na hali ya Ukame ambayo ni tatizo sugu katika maeneo mengi
nchini.
Kutokana na hayo DC Ndejembi ameagiza kuwa na kilimo cha Mtama zaidi
kuliko Mahindi. Kwani Wilaya ya Kongwa ina Kaya 59141, na kila kaya kama
ikilima Heka mbili (2) za Mtama, Mavuno itakuwa Tani 71000, za Mtama
sawa na 83% ya hitaji la chakula Wilayani Kongwa.
Katika
kukabiliana na njaa mahitaji mengine mahususi yametajwa ikiwa ni pamoja
na Kuongeza uzalishaji wa mtama toka tani 1/ Hekta mwaka 2016 hadi
tani3/hekta ifikapo mwezi June 2021, Kuongeza Uzalishaji wa Muhogo
mbichi toka tani 6/hekta Mwaka 2016 hadi tani 10 hekta mwaka 2029,
Kuongeza uzalishaji wa zao la Alizeti toka tani 1.2/ hekta mwaka 2016
hadi tani 1.8/hekta mwaka 2021.
Pia
Mhe Ndejembi alisema kuwa mahitaji mengine ni pamoja na Kuongeza
uzalishaji wa ufuta toka tani 0.5/hekta mwaka 2016 hadi tani 1.2/hekta
ifikapo june 2021, pamoja na Kuongeza pato la Mtu/watu toka Tsh
500,000/= Mwaka 2016 hadi Tsh 800,000/= June 2021.
DC
Ndejembi ameagiza kufanyika utaratibu wa kuhakikisha kila kaya
inalima Heka zisizopungua mbili (2) za Mtama, Mbili za Mahindi,
kulingana na eneo husika wakishauriwa na maafisa ugani lakini mtama ni
lazima kwa kila kaya hata kama analima mahindi.
Pia
amewaagiza vijana wote wasio na kazi Wilayani Kongwa wapewe Hekari mbili
kila mmoja ili waache kucheza pool table na kujihusisha na vikundi Ovu
vya wizi na matumizi ya Dawa za kulevya.
Saambamba
na hayo Mhe Ndejembi aamepiga marufuku kuchezwa mchezo wa Pool Table
mpaka ifikapo majira ya saa 10 jioni, hivyo kwa yeyote atakaye kiuka
utaratibu huo atakuwa amekiuka amri halali ya serikali.