WANAFUNZI WATAKIWA KUJIFUNZA UJASIRIA MALI MUSOMA MKOANI MARA

  wanafunzi shule 16 za sekondari musoma makini kusikiliza semina ya ujasiriamali iliyotolewa na mratibu Alex Mugabo wa mradi wa jpange kufanikiwa somo likiwa nguvu ya akili yako iko ndani ya mawazo yako
.

.......................................................
WANAFUNZI 370 katika shule mbalimbali za sekondari manispaa ya Musoma mjini wanaotarajia kumaliza kidato cha nne baadae mwaka huu wametakiwa kuwa chachu ya mabadiliko kwa kubuni miradi kuanzisha biashara sambamba na hilo kuendeleza elimu ya ujasiriamali nchini.


Badala ya kusubiri ajira ili waajiriwe wameelezwa kujenga dhana ya kujiajiri wenyewe katika akili zao na hili ni baada ya kuhitimu elimu hiyo,kutokukaa nyumbani kusubiri matokeo bali wawekeze katika ujasiriamali mafunzo waliyopata kupitia mradi wa jipange kufanikiwa.


Kauli hiyo ilitolewa juzi na mkurugenzi wa taasisi ya Tanzania Enterprenurs supporting centre ambayo inafanya shughuli ya kukuza ubunifu na kuendeleza ujasiriamali nchini Boniphace Ndengo katika sherehe ya kuwaaga wahitimu hao ambapo walikabidhiwa vyeti vya elimu ya ujasiriamali.


Alisema taasisi hiyo imeanzisha klabu ya jipange kufanikiwa mradi maaluum unaotoa elimu ya ujasiriamali kwa wanafunzi katika shule 16 za manispaa hiyo ili ,kujenga nchi na kutengeneza wajasiriamali watu mahiri katika ubunifu na ujasiriamali.


‘’Naamini kwamba wajasiriamali ndio mtaji ambao taifa linahitaji kujenga maendeleo hasa ya kiuchumi mtakumbuka tunapojifunza zile rasilimali za uzalishaji yako makundi manne ardhi,watu,mtaji lakini kuna kundi linaitwa wajasiriamali lianalounganisha hizi rasilimali zingine ili ziweze kufanya uzalishaji kwa hiyo tukaona kuna upungufu wa wajasiriamali nchini’’alisema Ndengo.


Kwa upande wake mwalimu wa biashara shule ya sekondari Morembe Bestina Msilanga alisema serikali ifikirie kuanzisha elimu ya ujasiriamali kama somo linalojitegemea na kwamba lianze kufundishwa katika shule ya msingi mpaka vyuo vikuu ili nchi iweze kujitegemea kwa kutumia pato lake la ndani ambalo ndio wajasiriamali.


‘’Tunawashukuru sana walioanzisha mradi wa jipange katika shule zetu elimu hiyo itamsaidia mtoto katika miaka ijayo kuweza kujitegemea kwa kufungua kampuni,kiwanda chake hatimaye kulipa kodi kubwa serikalini  mwisho wa siku serikali itaweza kujiendesha yenyewe bila kusubiri misaada toka nje ya nchi’’alisema .


Peter Nungu ni miongoni mwa wanafunzi hao alisema elimu ya ujasiriamali imemuwezesha kupata maarifa makubwa kiasi cha kupanua uelewa wake kutumia fursa mbalimbali zinazomzunguka ili aweze kufanikiwa pia anafikiria kujitegemea kwa kubuni biashara baada ya kuhitimu kidato hicho.


Powered by Blogger.