MISIMU MITATU NA ROBO, TAMBWE KATUPIA MABAO 60 LIGI KUU BARA, KICHUYA ANAWEZA KUJIFUNZA
TAMBWE |
PICHA NA SALEHE JEMBE
KAMA
Kocha Juma Mwambusi angeanza na mshambuliaji Amissi Tambwe katika mechi
dhidi ya JKT Ruvu, hakika habari ingekuwa nyingine kabisa.
Katika
mechi hiyo, Yanga ilishinda kwa mabao 4-0, lakini Donald Ngoma, Obey
Chirwa, Thabani Kamusoko na Simon Msuva walipoteza zaidi ya nafasi sita
za wazi za kufunga.
Tambwe
ni muuaji unapozungumzia suala la kufunga, hataki utani na katika
nafasi nne anaweza kupoteza moja na kufunga tatu. Hakika ni kati ya
washambuliaji wenye kipaji cha juu cha kufunga au umaliziaji.
Wakati
Ligi Kuu Bara msimu wa 2016-17 inaanza, ilionekana kama vile makali
yake yameisha licha ya kwamba katika misimu miwili iliyopita tayari
alikuwa mfungaji bora mara mbili. Na msimu mmoja akawa katika nafasi ya
pili.
Kocha
Hans van der Pluijm amerejea Yanga baada ya uongozi wa klabu hiyo,
kuukataa uamuzi wake wa kutangaza kujiuzulu. Maana yake bado Tambwe ana
nafasi ya kuendelea kufanya vema kama ataendelea kumpa nafasi ya
kutosha.
PICHA NA SALEHEJEMBE
KICHUYA |
Kwa
sasa Tambwe anaonekana kuwa katika kiwango bora zaidi baada ya
kufikisha mabao matano kwa mabao aliyofunga katika mechi tatu tu za
ligi. Alianza Septemba 10 wakati Yanga ilipoitwanga Majimaji kwa mabao
3-0, yeye akafunga mawili.
Septemba
17, Yanga ikiwa ugenini mjini Shinyanga ikashinda kwa mabao 2-0, Tambwe
tena akafunga na kuonyesha si mtu wa mchezomchezo.
Oktoba
Mosi, akafunga bao dhidi ya Simba ambalo lilizua utata mkubwa. Baada ya
hapo, mwendo wake ukawa wa kusuasua hasa baada ya kuumia.
Lakini
aliporejea, mechi ya kwanza aliingia dhidi ya Kagera Sugar, Yanga
ikishinda kwa mabao 6-2, hakufanya lolote. Mechi iliyofuatia dhidi ya
JKT nayo aliingia akapachika mabao mawili ya haraka na kusaidia ushindi
wa mabao 4-0.
Sasa
Tambwe ana mabao sita, moja pungufu dhidi ya kinara wa ufungaji mabao
kwa sasa. Huyu ni Shiza Kichuya, Mtanzania pekee anayeonekana kuwa na
kasi kubwa katika ufungaji wa mabao.
Kichuya
ameiongoza Simba vema na ilionekana kasi yake ni gumzo, lakini mwendo
wa Tambwe tayari umezua hofu na huenda unaweza kusababisha Kichuya
kutotulia kama asipousoma mchezo mapema. Kwamba bado anatakiwa kusaidia
zaidi kuliko kufunga.
Katika
upachikaji mabao, Tambwe ni ‘Mnyama’, hataki utani na anapoingia
uwanjani anataka kufunga kweli. Kinachomsaidia, silaha tatu za mfungaji
mahiri anazo. Yaani ana uwezo wa kutumia vizuri mguu wa kulia, anaweza
kufunga kwa kushoto, halafu ni mshambuliaji hatari zaidi anayeweza
kufunga mabao ya vichwa.
Rekodi
za nyuma zinambeba Tambwe kama mshambuliaji hatari zaidi kwa misimu
yote mfululizo. Kwa kuwa amekuwa mfungaji bora mara mbili, mara moja
kashika nafasi ya pili.
Utaona
katika Ligi Kuu Bara kwa misimu mitatu na robo, tayari amepachika mabao
60 katika ligi tu, huyu si mtu wa kawaida na kupambana naye inatakiwa
ubunifu mkubwa na nidhamu ya hali ya juu.
Mabao
19 alifunga katika msimu wa kwanza akiwa Simba, akaibuka kuwa mfungaji
bora, msimu uliofuata, bao moja akafunga akiwa Simba, 13 akafunga akiwa
Yanga na kumaliza msimu akiwa na mabao 14 na msimu uliopita akawa
mfungaji bora tena akiwa mabai 21.
Msimu
huu ambao kwake amecheza robo ya msimu ambao mechi hadi saba, tayari
ana mabao sita na kama hajaumia, hakika ataendelea kufunga zaidi.
Katika
misimu yote mitatu, kila mmoja alipiga hat trick moja au mbili.
Hajafanya hivyo msimu huu na inaonekana kwa anavyokwenda kuna uwezekano
mkubwa wa kufanya hivyo.
Nimekuwa
nikieleza kila mara, kwamba Tambwe ni mchezaji tofauti kabisa kati ya
wengi waliowahi kucheza soka nchini. Pamoja na kuwa na kipaji cha juu,
lakini ana nidhamu ya juu pia.
Kuweka
kipaji bora na nidhamu sahihi, hakika jibu ni maendeleo. Hiki ndicho
kitamsaidia na inawezekana ikawa ni vigumu au kazi ngumu sana kwa
Kichuya kupambana na Tambwe hasa ukizingatia sasa anaonekana kuwa ‘on
fire’.
Kama
Kichuya atanuia na kupambana naye, itakuwa ni changamoto na mafunzo
makubwa yanayoweza kuinua kiwango chake zaidi katika ufungaji kuliko
alivyo sasa.
Tambwe:
2013/14 mabao 19
2014/15 mabao 14
2015/16 mabao 21
2016/17 mabao 6
MECHI ALIZOFUNGA MSIMU HUU…
2016/17
Septemba 10, 2016
Yanga 3-0 Majimaji FC Taifa
Kaseke 19
Tambwe 79
Tambwe 84
Septemba 17, 2016
Mwadui FC 0-2 Yanga Kambarage
Amissi Tambwe 5
Donald Ngoma 94
Oktoba 1, 2016
Yanga 1-1 Simba Taifa
Tambwe 26 Kichuya 87
Oktoba 26, 2016
Yanga 4-0 JKT Ruvu Taifa
Obrey Chirwa 6
Amissi Tambwe 63
Simon Msuva 82
Amissi Tambwe 90