AUAWA KWA KUMWAMBIA MWENZAKE HAJATAIRIWA
picha siyatukio lenyewe;
Tarime. Mkrurya bana eti hataki hata matani! Watu wawili wamefariki dunia Wilayani hapa mkoani Mara kwa matukio mawili tofauti huku mwingine akidaiwa kuuawa kwa kumwita mwenzake hajatahiriwa kwa kilugha (Mrisiya).
Kamanda wa polisi Tarime Rorya Kamishina msaidizi Andrew Satta amemtaja aliyefariki kuwa ni Chacha Samwel Muniko 31 mkazi wa kijiji cha Nyangoto aambaye Oktoba 24 majira ya saa saba mchana katika kitongoji cha mjini kati Nyangoto alichomwa kwa kitu chenye ncha kali upande wa kushoto wa kifua na Benjamini Marwa Gabungwe 20 mkazi wa kijiji cha Kerende kwa kuitwa Mrisiya na kufariki dunia.
Kamanda alisema kuwa chanzo cha kifo cha Muniko ni yeye marehemu kumtania Gabungwe kuwa hajatahiriwa yaani yeye ni mrisha kitendo ambacho kilimfanya akasirike na kufikia hatua ya kumjeruhi na kumsababishia mauti.
Hata hivyo mtuhumiwa alikamatwa na na jeshi la polisi ambapo baada ya mahojiano kukamilika atafikishwa mahakamani kujibu shitaka hilo huku mwili wa marehemu ukiwa umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika kituo cha afya Nyamongo.
Katika tukio lingine Satta alisema kuwa Muhere Muhere Marwa ( 28) mkazi wa kijiji cha Genkuru alikutwa amekufa maji kwenye shimo la dhahabu la Nyabigenalinalomilikiwa na kampuni ya Acacia North Mara lisilotumika kwa sasa kwa shughuli ya uchimbaji wa madini.
Kamanda alisema kuwa mwili wa Muhere uliokotwa Oktoba 16 majira ya saa tisa 9:10 alasiri huku akitaja chanzo cha kufariki kwake kuwa ni kutafuta mawe yadhaniwayo kuwa ya dhahabu kwa ajili ya kujipatia kipato ambapo alizama maji yaliyokuwa yamejaa kwenye shimo hilo na kufariki duinia.
Kamanda alisema kuwa ukio lingine lilitokea Oktoba 24 saa 7:00 mchana katika kitongoji cha Nyamanche, kijiji cha Nyakunguru Wilayani hapa kwa Mery Baru Munge 40 kuchomwa kisu na jirani yake chacha Mseti Mang’era 32 wakati akiamua ugomvia baina ya mtoto wake Bahati Baru 16.
Munge alikutwa na hali hiyo wakati akiamua ugomvi kati ya mwanaye ambapo alichomwa kisu kitovuni na kumsababishia hali mbaya hadi kulazwa katika hospitali ya Wilaya ya Tarime.
“Alifika nyumbani kwake akiwa na kisu tayari kupambana na kijana wake huyo aliyemjeruhiwa kwa kmchoma kisu tumboni chini ya kitovu. Chanzo ni kuamua ugomvi baina ya mtoto wake na jirani yake huyo ulioanzia kwenye ulevi wao kwenye vilabu vya pombe za kienyeji ambapo mtuhumiwa aliambiwa kuwa ni mjinga na mtoto huyo majeruhi mwenye miaka 16,”alisema Kamanda Satta.