BARAKI SISTERS FARM YA PONGEZWA KWA MRADI WAKE WAKUIMARISHA HAKI ZA WANAWAKE WALIOATHIRIWA NA UKATILI WA KIJIINSIA UNAOTEKELEZWA RORYA.KWA USHIRIKA WA THE FOUNDATION FOR CIVIL SOCIETY.

Pichani ni Kaimu Afisa Elimu Bi. Joyce Tongori akifungu kongamano la shule za sekondari na Msingi lilloandaliwa na baraki sisters Farm kwa ushirika wa The Foundation for civili Society katika shule ya sekondari.
Sehemu ya wanafunzi wa shule ya Msingi Kines wakiimba nyimbo za uumbe wa kuitaka serikali kuwasaidia watoto kuachwa kukeketwa.
Majaji wakiandika maks kwa ajili ya shule inayofanya vizuri katika bonanza hilo kushoto ni Mchungaji .Elinafika Molel mratibu wa Dawati la Utetezi KKKT Marakushoto kwake ni afisa maendeleo Rorya Mwema SAlm, kushoto kwake Joyce Togori na kushoto kwake ni afisa utamaduni rorya.
Sehemu ya wazee wa kata ya Komuge waliofika katika bonanza hilo wakifatilia kwa umakini.
Sister Frorence Bhoke akimkabidhi Zawadi mmoja wawanafunzi walioimbuka washindi katika kongamano.
Katikati ni Mwema Salum Afisa maendeleo ambaye pia ni Mratibu Dawati la jinsia Rorya na Kushoto kwake ni Mwalimu Joyce kaimu Afisa Elimu Rorya. kushoto ni Mchungaji Mollel Mratibu wa Dawati la Utetezi KKKT Mara.
PICHA NA MAKALINEWS.
Wanafunzi wakiigiza Namna Mtoto wakike anavyolazimishwa hadi kukekeketwa.
Mr mgimba Mratibu wa Mradi
Shommi Binda mwandishi wa habari wa Gazeti la mtanzania Mara akiionesha uhodari wa kuimba ushairi katika kongamano hilo naye pia nimwanamalenga.
Shommi Binda mwandishi wa habari wa Gazeti la mtanzania Mara akiionesha uhodari wa kuimba ushairi katika kongamano hilo naye pia nimwanamalenga.
Diwani wa kata ya Komuge WiliamNestory akitoa neno katika kongamano .
Zawadi zilizoandaliwa kwaajili ya washindi,
Sister. Frorence Bhoke akitoa Neno wakati wakufunga Kongamano hilo.
Zawadi zikiendelea.
PICHA ZOTE NA MAKALINEWS.
Serikali wilayani Rorya Mkoani Mara imeupongeza mradi wa wa kuimarisha haki za wanawake walioahiriwa na ukatili wa kijinsia ikiwemo ukeketaji katika mkoa wa mara.
Akizungumza katika kongamano la shule za sekondari na msingi lililoandaliwa na na Baraki Sisters Farm kwa ufadhili wa wa the foundation for civili society kaimu afisa elimu Bi.Joyce Tongori alisema mradi huo umekuwa chachu kubwa yakuondoa vitendo vya ukatili katika wilaya hiyo japo bado vitendo hivyo vinaendelea chini kwa chini.
Pia aliyataka mashirika hayo kujitokeza kwa wingi huku wakiahidi kutoa ushirikiano mkubwa kwao.
Naye afisa maendeleo ambaye pia nimratibu wa Dawati la jinsia wilayani rorya Mwema salum alisema hali bado nitete katika wilaya hiyo japo elimu inatolewa kwa kasi kubwa huku akisema watahakikisha wanaondoa dhana potofu iliyojengaka katika jamii kuhusiana na ukatili hususani ukeketaji.
Aidha sisiter frorence ambaye pia ni nmwezeshaji katika mradi wa Baraki sisters Farm alisema wamefanikiwa kwa kiasi baada ya kuwatumia wazee wamila kwani wao ndio wenye sauti katika jamii kuwa elimu na sasa wanajivunia kwa elimu amabayo wameifikisha imesaidia japo bado wataendelea zaidi kutoa elimu kuhusian na ukatili wa kijinsia.
Kongamano hilo limeenda sambamba na michezo mbalimbali zikiwempo nyimbo ,ngojera ,maigizo huku zikitolewa zawadi kwa washindi wa shule zilizoibuka washindi.
KWA TAARIFA ZOTE SIKILIZE VIDEO HAPO CHINI