MATUKIO TOFAUTI YA PICHA KATIKA MCHEZO WA MWISHO WA BIASHARA UNITED ULIOIPELEKA LIGI KUU MSIMU UJAO.



kikosi cha Biashara United mara pamoja na viongozi mbalimbali aliyevalia miwani ni mkuu wa mkoa wa mara Adam Malima.


Sehemu ya mashabiki wa mpira mkoani mara wakifatilia mtanange huo katika uwanja wa Karume mjini Musoma.
Shemu ya mashabiki wa soka mkoa wa mara waliojitokeza kuipa nguvu timu yao katika mchezo wa mwisho

Timu ya Biashara United Mara hatimaye imepanda ligi kuu msimu ujao baada ya ushindi wa Nyumbani wa mabao 3 kwa 2dhidi ya TRANS CAMP katika mchezo uliopigwa kunako dimba la karume mjini Musoma mkoani mara.

Biashara United Mara kwa mara ya kwanza ikishika nafasi ya polisi mara imekata kiu ya wana mara baada ya kupanda ligi kuu kwa takribani miaka 15 wakazi wa mkoa huo kutoiona ligi kuu ikishiriki katika mkoa huo hatimaye sasa wameuona mwezi.

Biashara imekuwa timu ya tano kupanda Ligi Kuu Bara na kuamsha shamgwe kubwa kwa mashabiki na wapenzi wa mpira wa mkoa huo.

Alikuwa ni Songa Bethel baada ya kuangushwa kwenye penalt nakuamuliwa kupigwa mkwaju huo kunako dakika ya 59 ya mchezo na Sospeter Maiga nakuisawazishia biashara nakufanya ubao kusomeka 1vs 1 ili wachukua Biashara kunako dakika ya 32 kunako kipindi cha pili Biashara wakaandika bao la pili kupitia yule yule aliye wapandisha singida united Songa Bethel nakuwafanya kutangulia biashara kijana masoud dakika za lala salama akawandikia biashara bao la 3 na laushindi nakuwafanya kutoka kifua mbele.


Biashara imefanikiwa kupanda baada ya kuitwanga Transit Camp kwa mabao 3-2 katika mechi kali mjini Musoma, Mkoani Mara

Ushindi huo unaifanya Biashara kufikisha pointi 30 na kubaki kileleni mwa Kundi C ikifuatiwa na Alliance.

Wenyeji Biashara walilazimika kufanya kazi ya ziada kupata mabao ya haraka baada ya timu hizo kushindwa kufungana mapema.

Timu nyingine nne zilizopanda Ligi Kuu Bara ni pamoja na JKT Ruvu iliyokuwa ya kwanza, KMC ya Dar es Salaam, Coastal Union ya Tanga, Alliance ya Mwanza na Biashara.

Sasa imebaki timu moja inayotafutwa kukamilisha idadi ya timu sita zinazotakiwa kupanda ligi kuu msimu ujao.
Baadhi ya wachezaji wa timu ya Biashara United


Umati wa Mashabiki waliojitokeza uwanjani katika kuiunga mkono timu ya biashara United

MASHABIKI wa timu ya Biashara United ya mkoani Mara, wakifanya shangwe kwenye uwanja wa kumbukumbu ya Karume mjini Musoma baada ya kuifunga timu Trans campa ya mjini Shinyanga bao 3-2 na kujihakikishia ushindi wa kupanda ligi kuu soka Tanzania Bara kwa msimu wa 2018/ 2019.
Powered by Blogger.