ILIVYOKUWA KESI YA KUJIUNGANISHIA BOMBA LA MAFUTA YA DIZELI NYUMBANI
Mfanyakazi
Mstaafu wa Shirika la Mafuta Tanzania na Zambia (TAZAMA) Samwel
Nyakirang’ani (63) na wenzake wanaokabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi wa
kujiunganishia Bomba la Mafuta ya Dizeli wameiomba Mahakama ya Hakimu
Mkazi Kisutu, iwapatie dhamana.
Maombi
hayo wameyawasilishwa kupitia Wakili wao, Kusalika Augustine mbele ya
Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba ambapo alidai wateja wake wanahitaji
kupata dhamana kwa sababu mashtaka yanayowakabili yanadhaminika.
Kutokana
na maombi hayo, upande wa mashtaka uliomba kesi hiyo iahirishwe ili
wajibu hoja hizo, ambapo Hakimu Simba aliahirisha kesi hiyo hadi
February 22, 2018.
Washtakiwa
wengine katika kesi hiyo ni Nyangi Mataro ambaye ni Mwalimu wa Shule
ya msingi Ufukoni na mkazi wa Kisiwani Mkajuni Kigamboni.
Wengine ni Mfanyabaishara, Farijia Ahmed, Malaki Mathia, Kristomsi Angelus, Pamfili Nkoronko na Hunry Fredrick.
Kwa
pamoja washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka matatu ya uhujumu uchumi
kwa kujiunganishia isivyo halali Bomba la Mafuta ya Dizeli, kinyume
cha sheria ya Uhujumu uchumi.