MAKALINEWS.PROF.SOSPETER MUHONGO AONGEZA NGUVU UJENZI WA ZAHANATI YA NYASAUNGU.

Sehemu ya wananchi na viongozi wa jimbo wakiwemo madiwani na Mbunge wa jimbo
la musoma vijijini Prof.Sospeter Muhongo wakiwa katika picha ya pamoja.

katikati Ni mbunge wa Prof. Muhongo kushoto kwake akitoa maelekezo kwa Fundi aliyechukua dhamana ya kujenga Zahanati Ya Nyasaungu.

Diwani wa kata ya Ifulifu Manyama Meru akizungumza katika mkutano wa Hadhara.

Aliyevalia Tsheti ya Blue ni mbunge wa musoma vijijini akikagua ujenzi wa Zahanati.



Kaimu Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Musoma Vijiji Dr.Thadeus Makwanda akizungumza katika mkutano.
**MAKALINEWS** MARA.
Wananchi wa kijiji cha Nyasaungu katika Halmashauri ya wilaya ya Musoma Vijijini
mkoani Mara wamefanikiwa kupata zaidi ya mifuko 200 ya saruji
itayosaidia kuendeleza ujenzi wa kituo cha afya kilichokuwa kimesimama
takribani miaka mitatu kutokana na ukosefu wa fedha.
Kupatikana kwa mifuko hiyo kumetokana na ziara za mara kwa mara zinazotekelezwa na
mbunge wa wilaya hiyo Sospeter Muhongo ambaye amekuwa akitembelea
miradi mbalimbali ya maendeleo inayofanyika kwa nguvu za wananchi,
ambapo jana alikutana na wakazi wa kijiji hicho na kufanya harambee
kukusanya fedha zitazotumika kununua mifuko hiyo iliyochangiwa na
madiwani, viongozi mbalimbali wa halmashauri hiyo na wananchi wenyewe.
Awali mwenyekiti wa kamati ya ujenzi wa zahanati hiyo Magesa Chacha alisema
shughuli za ujenzi zilianza mwaka 2012 kuweka msingi lakini baadae
Halmashauri walipima eneo lile na kubomoa msingi mwaka 2014 kutokana na
sababu za kitaalamu za uhandisi ndipo wakahamia eneo jingine na
kufanikiwa kujenga msingi baada ya kupata maelekezo kutoka halmashauri.
wamekuwa wakitembea umbali mrefu mpaka kata ya Nyakatende na Nyasurula
“Wananchi kwa ajili ya kufuata matibabu lakini pia tulijitahidi kujenga zahanati
ya Kiemba kwa kushirikiana na wilaya ambapo pia iko mbali na kijiji
hiki, sasa hii zahanati ya Nyasaungu itakuwa karibu sana tumekusanya
mawe, mchanga lakini tunakabiliwa na ukosefu wa mifuko ya sementi zaidi
ya 150 ili kuanza ujenzi”alisema.
Kufuatia uwepo wa changamoto hiyo ya saruji Mbunge wa jimbo hilo Sospeter Mhongo aliyekuwa
ameambatana na madiwani wa kata mbalimbali wilayani hapa alilazimika
kuendesha harambee ili kuchangia upatikanaji wa idadia mifuko hiyo
ambapo alifanikiwa kutoa mifuko 100 ya saruji papo hapo.
Aidha alitoa agizo kwa mganga mkuu wa wilaya hiyo kuwa ifikapo jumamosi ya
wiki ijayo aweze kwenda eneo la ujenzi wa zahanati hiyo akiwa na
mkandarasi mzoefu wa Halmashauri atakaye toa maelekezo ya kazi kwa fundi
husika wa jengo hilo pia aliwataka wananchi hao kuandaa ratiba za
mkandarasi huyo kutembelea na kukagua maendeleo mbalimbali vya ujenzi wa
zahanati hiyo waliyokubaliana ifikapo june 30 mwaka huu iwe
imekamilika.
“Baada ya hapo ikishafika tarehe 30 ya
mwezi wa sita mwaka huu Boma limekamilika tutakuja tena,tutakuwa na
Halmashauri tutakuja kujadili tunaliezekaje sawa kama ni halmashauri
tutaiomba iezeke kama haiwezi tutatumia njia nyingine mimi nawaomba
madiwani na mwenyekiti wa halmashauri wawe wanafika kukagua maendeleo ya
ujenzi wa zahanati yetu na tarehe hiyo mganga mkuu wa wilaya atakuja
ameandaa taratibu za usajili ili tujue itaanza kazi lini baada ya
kuezekwa”alisema.
Naye mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Charles Magoma aliwataka wananchi kutoacha kuwekeza
nguvu zao katika miradi mbalimbali ya maendeleo kijijini hapo kwakuwa
wao ndio wanufaika sambamba na hilo serikali inapeleka huduma za
maendeleo kwa jamii katika maeneo mengi ukizingatia jimbo hilo
kukabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo tatizo la vyumba vya madarasa na
hilo la afya katika maeneo mengine.
TIZAMA VIDEO HII UONE KILICHOZUNGUMZWA KATIKA ZIARA YA MBUNGE HUYO.