CHADEMA KUFIKISHA MALALAMIKO SITA KWA MKURUGENZI NEC, WATAKA MAJIBU LEO


Chama cha Chadema kimesema kinapeleka malalamiko sita kwenye Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kama walivyoelekezwa na Mkurugenzi wake, Ramadhani Kailima kwa ajili ya kutafutia suluhuhisho.

Akizungumza na wanahabari leo baada ya kuongea kwa njia ya simu na Kailima katika Ofisi za NEC, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema tume hiyo inatakiwa itoe mapema majibu ya malalamiko hayo, ili kuondoa uwezekano wa kuvurugika uchaguzi wa Jimbo la Kinondoni.

“Tuliona kuna mambo inabidi tupate mazungumzo na NEC baada kuona mawasiliano yetu na tume yako taratibu, muda wa kuelekea uchaguzi Jumamosi unakaribia na tuliona mapungufu kadha wa kadha. Tukaona tuwasiliane na tume, tumezungumza na Kailima kwenye simu kuhusu malalamiko tuliyo nayo,” amesema na kuongeza.
“Tuna malalamiko karibu sita, tunahitaji tume itupe majibu yake mapema iwezekanavyo ili kuondoa uwezekano wa kuvurugika uchaguzi wa kinondoni. ameahidi anawasiliana na wenzake ikiwemo mkurugenzi wa kinondoni kuona watasema nini na akasema atanijibu kwa maandishi na kwenye simu na kwamba leo jioni atatupa majibu.”
Mbowe ametaja malalamiko hayo ikiwemo, Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni kutowaapisha mawakala wa ziada pamoja na kukataa madiwani, wabunge na viongozi wa Chadema kuwa mawakala licha ya sheria kuruhusu hilo kufanyika.
Malalamiko mengine, tamko la Mkurugenzi la kutaka mawakala wote kuwa na vitambulisho baada ya kuapishwa, kutotolewa kwa hati za viapo kwa baadhi ya mawakala, pamoja na kubadilishwa kwa eneo la majumuisho ya kura.
Pia amesema “tuna taarifa zenye uthibitisho kwamba walioteuliwa Kinondoni kuwa wasaidizi wa uchaguzi katika vituo vya kupigia kura wanatoka Ilala na Temeke, wengine ni viongozi CCM, wengine wa serikali,  tunamwambia orodha hii iwe wazi leo ili tujue kama kuna msimamizi kada tumuwekee pingamizi.”
Powered by Blogger.