CHAMA CHA RIADHA MANISPAA YA MUSOMA MWENDO MDUNDO;
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara Samweli Kiboye no 3 akikabidhi Zawadi kwa washindi wariadha ambao ni Wanafunzi wa shule za sekondari. |
Sehemu ya Wanariadha hao mara baada ya kukabidhiwa Zawadi zao. |
Mwenyekiti wa Cha cha Riadha Manispaa EVA Msiba alivyohudhuria katika sherehe za miaka 41 ya kuzaliwa chama cha mapinduzi. |
Mwenyekiti wa CCM Mkoa akiendelea kukabidhi zawadi aliyevalia kofia ku;lia kwake ni mwenyekiti wa CCM Wilaya Bwana Magili shati ya njano ni Mkuu wa Mkoa Wa Mara Adam Malima. |
PICHA NA MAKALINEWS.
Na MAKALINEWS. MARA.
Chama cha Riadha Manispaa ya Musoma kimefanya Bonanza ambalo limehusisha vijana kutoka shule mbalimbali za sekondari na msingi mkoani mara huku lengo ikiwa nikufufua mashindano ya Riadha nakuwajenga vijana kuupenda mchezo huo.
Bonanza hilo lilienda sambamba na maadhimisho ya miaka 41 ya kuzaliwa kwa chama cha mapinduzi ambapo kimkoa yamefanyika katika kata ya mwisenge mjini Musoma.
Akizinguzumza mara baada ya kuhitimisha mbio hizo mwenyekiti wa CCM wilaya ya Serengeti Mkoani Mara Jacob Bega alisema niwakati sasa umefika kuifufua michezo hiyo ilikuwapa fursa vijana.
Naye mwenyekiti wa chama hicho Eva msiba alisema bonanza hilo nisehemu ya maandalizi ambapo sasa lengo nikuandaa vijana kwa ajili ya kuwajenga nakuzifikisha ndoto zao panapotakiwa.
Bonanza hilo limeshirikisha mbio mita 100,400,8000,1500 huku huku shule miongoni mwao iukiwemo makoko day,zikibuwa washindi hao.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara mbunge wa jimbo la Musoma mjini vedastus manyinyi mathayo alisema kila kikundi kijiandae kwani sasa wanaenda kuibua michezo yote ikiwemo Riadha ,mpira wa miguu,pete,namichezo mingine.