WAZAZI WAWASHAWISHI WANAFUNZI KUFELI MITIHANI ILI WAOLEWE




Mwenyekiti wa kijiji Cha Mwamanimba Patrick Lutego akiongea na wazazi, walimu na wanafunzi wa shule ya Msingi Mabambasi katika kikao kilichofanyika shuleni hapo mwishoni mwa wiki jana kwa ajili ya kujadili juu ya ufaulu wa wanafunzi shuleni hapo.

Shule ya Msingi Mabambasi iliyoko wilayani Meatu mkoani Simiyu.A




Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mabambasi iliyoko wilayani Meatu mkoani Simiyu, Samsoni Tingo akiongea na wazazi, kamati ya shule, walimu, maafisa elimu na wanafunzi katika kikao cha kujadili mikakati ya ufaulu wa wanafunzi shuleni hapo.
Na Makaliblog.simiyu
WAZAZI wa wanafunzi wa shule ya Msingi Mabambasi wilayani Meatu mkoani Simiyu wamekuwa chanzo cha kufeli kwa watoto wao katika mtihani wa darasa la saba mwaka huu ili watoto hao wachunge na kuolewa.

Jamii hiyo ambayo ni ya wafugaji wamejenga dhana juu ya urithi wa mtoto ni mifugo na kupata familia badala ya elimu, kwa sababu hata wachache wanaofaulu huzuiwa kuendelea na masomo.

Akitoa taarifa ya ufaulu wa shule hiyo Samsoni Tingo ambaye ni Mwalimu mkuu, alisema kuwa mwaka 2013 walihitimu wanafunzi 29, akafaulu 1, 2014 walihitimu 19 alifaulu 1, 2015 walihitimu 21 alifaulu 1, 2016 walihitimu 19 walifaulu 4 na mwaka 2017 walihitimu 20 hakuna aliyefaulu.


Tingo alisema kuwa wamebaini wazi kuwa wazazi wa wanafunzi hao huwashawishi wanafunzi wao kufanya vibaya mtihani wa mwisho ili wafeli baadae wakaolewe na kuchunga mifugo.

Aliongeza kuwa kuna baadhi ya watoto waliokuwa wanawaamini ni wazuri, lakini katika mtihani wa mwisho wamefanya vibaya sana na kungeza kuwa mahusiano yao na jamii siyo mazuri.


‘’tunasikitika sana kwa nini hawa wazazi wanfanya hivyo, Dilu Ngusa alikuwa akishikna nafasi ya kwanza kila mwaka, lakini mtihani wa mwisho kafanya vibaya zaidi na kushawishi na wenzake hali iliyosababisha hadi kuharibu miundombinu ya shule…Ngollo Mipawa alifaulu lakini wazazi wake walimshawishi kuacha shule ili aolewe’’ alisema Mwalimu Tingo.

Kwa upande wake kaimu Afisa Elimu wilayani humo John Mpamwa alisema kuwa ni dhahiri watoto hao hukanywa na wazazi wao kufanya vibaya katika mtihani wa mwisho ili wasifaulu kuendelea na masomo.

‘’katika mtihani ya kawaida ya kata na Mock Mkoa wanafunzi wote 20 walifaulu sana, lakini kwa nini katika mtihani wa mwisho wamefeli wote?...tufike mahali wazazi tujitafakari upya, ufugaji hauwezi kumzuia mtoto kuendelea na masomo na kufanya hivyo mnawaandalia maisha mabaya baadaye’’ alisisitiza Mpamwa.

Aliongeza kuwa baada ya matokeo kutangazwa yeye alifika shuleni hapo na kuwaita wanafunzi wote waliohitimu na kufeli, akatoa jaribio, zaidi ya wanafunzi 7 walifanya vizuri.


Dotto Miligwa ni mzazi wa wanafunzi shuleni hapo alisema kuwa ni kweli baadhi wazazi wanashawishi watoto wao kufanya vibaya ili wakachunge na kuolewa, tunajitahidi kuwashauri na kuwajengea ulelewa.


Naye Patrick Lutego Mwenyekiti wa kijiji cha Mwamanimba alisema kuwa jamii hiyo haina mwamko wa elimu, lakini kupitia matokeo hayo amejipanga kuhakikisha mwaka ujao wanafunzi wanafaulu.


Geni Majingwa (13) ambaye ni mhitimu wa shule hiyo kwa mwaka huu alisema kuwa siku za mtihani kulikuwa na makundi ya wanafunzi walikuwa wakishawishi tufanye vibaya na baada ya mtihani walirudi kuharibu mazingira ya shule yakiwemo mawe na milango ya madarasa.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Meatu Fabian Manoza anasema kuwa Mpango wa Kuinua Ubora wa Elimu (MKUE au EQUIP) imesaidia kuongeza ufanisi katika sekta ya elimu.


Alisema kuwa jamii wilayani humo ni ya wafugaji ambayo inathamini sana mifugo kuliko hata rasirimali watu, inaona kuwa kumpeleka mtoto shule aache kuchunga ni kupoteza muda.

‘’wafugaji wengi wanaishi kwa kuhamahama, hivyo tumeanza utaratibu wakuwapimia wafugaji maeneo yao ili wawe na makazi maalumu na pia kuwafundisha njia za ufugaji wa kisasa ili watoto wao waweze kuwa na makazi maalumu na waweze kundelea na masomo na pia kufanya vizuru katika mitihani’’ alisema Manoza.


Aliongeza kuwa wazazi hawana utamaduni wa kusomesha watoto, hali inayowafanya kudiriki kuwahimiza watoto waandike majibu ya uongo, hivyo wanao wajibu katika kuwabadilisha wafugaji hao.


Katika kikao kilichowakutanisha wazazi, wazee maarufu, viongozi wa dini na wa serikali, walimu na watendaji waliazimia kwa pamoja kuwa mikutano ya mara kwa mara, kuchangia chakula shuleni na ikiwezekana mwezi wa nane wanafunzi wawe kambi kwa ajili ya maandalizi ya mtihani hadi siku ya kuhitimu.

Shule Msingi Mabambasi iliyopo kjijiji na kata ya Mwamanimba imeshika nafasi ya mwisho kiwilaya kati ya shule 112, na nafasi ya mwisho kimkoa katika ya shule 8645, kwa sababu hakuna mwanafunzi yeyote aliyefaulu kwa kupata jumla ya alama 100.




Powered by Blogger.