Njia za kuwasaidia wanaume kukabiliana na upara




Tatizo la kunyonyoka kwa nywele na kuwa na kipara limekuwa likiwatatiza wanaume wengi kwa muda.

Shida hii mara nyingi huanza wanaume wakiwa wana miaka 30 hivi, na kufikia umri wa miaka 50 nusu ya wanaume huwa wanakabiliwa na tatizo hili.

Tatizo hili hutokana na vinyweleo vya nywele, ambavyo huwa kina cha ukuaji wa nywele, kujinywea. Shughuli hii huendelea pole pole kwa muda mrefu.

Kuna wengi wanaodai kuwa na tiba ya tatizo hili, baadhi wakitumia dawa za kisasa na wengine za kiasili lakini ufanisi wake huwa tofauti.

Ni njia gani hufanikiwa?

Kwa mujibu wa Idara ya Taifa ya Afya Uingereza (NHS) kupandikizwa kwa nywele ni moja ya njia zinazofanikiwa sana.

Lakini gharama yake huwa ya juu mno.

Kupandikizwa nywele kunaweza kugharimu kuanzia £1000 hadi £30,000.

Wakati mwingine, daktari wako anaweza kukupendekezea utumie dawa yenye kiungo fulani ambacho hujulikana kama Finasteride. Kiungo hiki hubadilisha viwango vya homoni fulani zinazodhibiti mfumo wa uzazi katika binadamu.

Utafiti unadokeza kwamba tiba hii inaweza kusisimua ukuaji wa nywele tena katika theluthi mbili ya wanaume wenye upara.

Dawa nyingine kwa jina Minoxidil iligunduliwa kibahati miaka ya 1950 watafiti waliokuwa wanatafuta tiba ya shinikizo la damu. Inaaminika kwamba hufanya kazi kwa kwa kuongeza mtiririko wa damu kwenye ngozi ya kichwa maeneo yenye nywele na kufungua vinyweleo vya nywele.

Ikitumiwa vyema, inaweza kufanikiwa kwa asilimia 80 ya wanaoitumia, lakini huhitaji kutumiwa kwa muda mrefu.

Kutumia dawa hizi mbili kunaweza kukugharimu maelfu ya pesa kila mwaka.
 cHANZO bbc.
Powered by Blogger.