WANANCHI WAANDAMANA KISA KUPANDA KWA BEI YA MKATE



Sudan imekumbwa na maandamano katika miji mbalimbali kutokana na ongezeko la bei ya mkate.
Habari zinasema gharama zimeongezeka mara mbili na sababu kubwa ni hatua ya serikali kuondoa ruzuku ya vyakula uamuzi ambao umesababisha bei ya mkate kuwa mara dufu.

Maandamano yaliyofanyika magharibi mwa Darfur yamesababisha mwanafunzi mmoja kuuawa na wengine sita kujeruhiwa baada ya kuzuka fujo.

Vyombo vya habari vimeripoti kwamba polisi walitumia mabomu ya machozi kutawanya watu ambao walikuwa wamefunga barabara na kuchoma matairi katika barabara za mji mkuu wa Khartoum.

Lakini naibu waziri wa mambo ya ndani alisema maandamano hayo hayakutokana na ongezeko la bei na akaahidi kuwashughulikia wote waliofanya maandamano yenye fujo. Pia, Serikali imezuia kuuzwa mitaani magazeti yote yaliyokosoa ongezeko la bei. Vyanzo vya uhakika vimezema uamuzi wa kuongeza bei ya mkate umefikiwa na serikali ikiwa ni utekelezaji wa matakwa ya kufufua uchumi yaliyotolewa na IMF.
Powered by Blogger.