MKUU WA MKOA WA MARA AWATAKA VIONGOZI KUSIMAMIA FEDHA ZA UMMA



VIONGOZI wa serikali mkoani Mara wametakiwa kuwa makini sana katika usimamizi wa fedha zinazotolewa na uongozi wa awamu ya tano, ili kutekeleza shughuli mbalimbali za miradi ya maendeleo kwa manufaa ya wananchi.

Rai hiyo ilitolewa Jana na mkuu wa mkoa huo Adam Malima alipokuwa anafungua kikao cha bodi ya barabara kilichofanyika katika ukumbi wa Uwekezaji, ambapo viongozi wa halmashauri za wilaya mbalimbali walihudhuria, wakandarasi waliohudhuria.

Alisema kikao hicho ambacho kwa Mara ya kwanza kilimeshirikisha wakala wa barabara za vijijini na mijini(Tarura)mkoani hapa ambao wanasaidiana majukumu na ofisi ya Meneja wa mkoa wa wakala wa Barabara(Tanroads).

Malima, Alitoa angalizo kabla ya wajumbe kuanza kujadili hali ya maendeleo ya miundombinu ya barabara kuwataka washiriki waliofika kwa lengo la kutimiza mkataba wa sheria kuondoka mapema kikaoni hapo ambapo hakuna aliyeondoka.

"Ni jambo ambalo linachukiza pale ambapo miradi ya umma inatolewa fedha lakini inashindwa kufika katika kiwango stahiki, kwa sababu hata ushiriki wenu unaonesha kama mmekuja kutimiza mkataba wa sheria inavyotutaka kufanya kikao cha bodi ya barabara kwa mwaka"alisema.

Aidha aliongeza kusema bunge la jamhuri ya muungano nchini katika malengo ya serikali ya awamu ya tano suala la miundombinu ya barabara, hali iliyojitokeza pia katika ilani ya uchaguzi ya chama cha mapinduzi(CCM) mwaka 2015.

Kwa kuzingatia hilo Meneja wakala wa barabara mkoani hapa Mhandisi Mlima Felix alisema katika mwaka wa fedha 2017/2018 jumla ya shilingi 21,501 milioni ziliidhinishwa kwa ajili ya matengenezo ya barabara.

"Katika fedha hizo serikali iliagiza kiasi cha shilingi 10,890 milioni zielekezwe kulipa madeni ya kazi za mwaka wa fedha 2016/17 na miaka mingine ya nyuma na kiasi cha shilingi milioni 10.6 ni kwa ajili ya kugharamia matengenezo ya barabara km 812.93 na madaraja 60 kwa mwaka wa fedha 2017/18"alisema.
Powered by Blogger.