Muuza ndizi wa miaka 94 aliyeporwa Indonesia achangiwa pesa
Watu nchini Indonesia wameungana
kumsaidia mzee mmoja muuza ndizi ambaye anasema kuwa aliiporwa zaidi ya
rupiah milioni 1 au dola 80
Suratman mwenye umri wa miaka 94, aliombwa na dereva mmoja aingie kwenye gari lake ili auze matunda.Akiwa ndani ya gari hilo wanaume hao walimlazimisha Bwana Suratman kutoa pesa zote kwa mfuko, kisha wakamtupa nje na kutoroka kwa gari lao.
Tommy Reza alichapisha video ya Bwana Suratman akiwa mwenye mawazo ambayo imevutia huruma na watu kutoa mchango.
Kisa hicho kilitokea mkoa wa Jambi katika kisiwa cha Sumtara. Tommy Reza aliambia BBC kuwa alimpata Bwana Suratman akiwa mwenye majonzi.
"Nilikuwa eneo hilo wakati nilimuona mwanamume akipiga kelele akiomba msaada," alisema Reza.
Tangua video hiyo iweke kwenye mitandao ya zaidi ya rupiah milioni 37, zaidi ya dola 2900 zimechangwa.
Gavana wa eneo hilo baadaye alitoa rupiah milioni 5. Kisha bwana Reza akachapisha picha akimkabidhi Suratman pesa hizo.