KIMENUKA.....WALIOFANYA UBADHIRIFU WA FEDHA IMARA SACCOS KUCHUKULIWA HATUA KALI ZA KISHERIA



Mwenyekiti Mpya wa Ushirika huo Bi Josephine Marcus akisoma Taarifa ya Fedha za Ushirika kabla ya Kuchaguliwa hii leo.

Richard Majalla Kaimu Mrajis wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Mara

katibu tawala wilaya ya musoma akizungumza katika mkutano mkuu wa chama cha imara sacoss mjini musoma mkoani mara





Wanachama wa Ushirika huo wakiwa katika Mkutano wa Mwaka.

Meneja wa Ushirika na Katibu wa Bodi Ellisha Obadia akieleza jambo katika Mkutano mkuu wa chama.
Aliyekuwa Kaimu Mwenyekiti wa Imara Saccos.Gideon Maberi akifafanua jambo katika Mkutano huo.







.......... ******...............

**Serikali ya mchunguza aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho kwa tuhuma za ubadhirifu wa fedha ;

Serikali mkoani mara imesema haitasita kumchulia hatua yeyote aliyehusika na ubadhiribu wa mamilio ya fedha katika chama cha ushirika na mikopo Imara saccos kilichopo wilayani Musoma Mkoani mara.


Chama cha ushirika wa akiba na mikopo imara saccos kilichopo mkoani mara kimegubikwa na wimbi la upotevu wa mali za chama hicho huku ukituhumiwa uongozi uliokuwa madarakani awali..

chini ya mwenyekiti wake bwana Bonphace ndengo.

Akizungumza katika kikao hicho katibu tawala wilaya ya musoma Bwana Justine manko awali aliwataka wanachama wa imara kuchagua viongozi wenye weredi ambao watashirikiana napo kufanya kazi za chama hicho.


Ambapo alisema miongoni mwavyma ambavyo vinafanya vizuri nichama cha imara saccos kutokana na kuwa na uongozi uliosimama nakuvizidi vyama vingine vya ushirika katika mkoa huo vinavyoshindwa kujiendesha kutokana na ugonzi mbaya.

Akiwa mwishoni kukamilisha hotuba yake kukaibuka swala la mwenyekiti wa Awali bwana Bonifance ndengo kutuhumiwa kwa ubadhirifu wa fedha za chama hicho ambapo swala hilo lilijibiwa na Bwana Richard majalla ambaye nikaimu mrajis wa vyama vya ushirika mkoani mara nakusema kuwa swala la mwenyekiti huyo tiari vyombo vya sheria vinaendelea kuchunguza na taarifa itatolewa.

Kwa mujibu wa mkutano huo ,Bwana ndengo anatuhumiwa kufanya ubadhirifu wa fedha za chama hicho huku akihusishwa kununua baadhi ya viwanja nje ya mkoa wa mara,katika wilaya ya Bariadi mkoani simiyu jambo ambalo chama hicho hakina hata tawi katika wilaya hiyo lakini alifanya hicho kwa matumizi mabaya tu ya fedha.

Katibu tawala amewatoa wasiwasi wanachama nakuahidi kumchukulia hatua kiongozi yeyeote aliyehusika na ubadhirifu wa fedha hizo.

naye kwa upande makamu mwenyekiti wa Imara Saccos.Gideon Maberi alisema nimatumizi makubwa na mabaya ya fedha yaliyofanyika katika chama hicho huku akiomba serikali kuchukua hatua kali kwa wahusika wote.

Aidha kwa upande wake meneja wa chama hicho cha imara saccos bwana Elisha Obadia alisema nivyema wananchama wakashikama kwa wakati huu kwa ajili ya kujenga nakukiendeleza chama nakuacha makundi, huku akiwaahidi wananchama waimara saccos kutokuwa nawasi wasi wowote kuhusian na pesa na hisa zao ziko salama sikama inavyodaiwa kuwa fedha za wananchama hazipo.

imara saccos inawanachana zaidi ya elf moja (1000) ambayo imeshirikisha vikundi mbalimbali vya kukopa nakuwekeza katika chama hicho.

Makaliblog ilipo mtafuta mwenyekiti aliyemaliza mda wake Bwana ndengo hakupatikana nahata alivyopigia simu hakuwa tiari kupokea simu yake.

Mkuatano mkuu umemchagua Bi.Josephine Marcus kuwa mwenyekiti wa chama cha Imara saccos,huku makamu mwenyekiti akiwa Bwana Gideoni Maberi ,huku wajumbe wa bodi Sara Bisanda,Michael Alen,Singo na George Misoke.

TOA MAONI YAKO MATUSI( HAPANA)

UNAWEZA KUTUPIGIA KUPITIA 0754295996
Powered by Blogger.