EQUIP ;IDADI YA WATOTO WASIO JUA KKK YAPUNGUA KATIKA HALMASHAURI YA TARIME MJINI
Idadi ya watoto wasio jua kusoma na kuandika wa darasa la kwanza mpaka la tatu katika Halmashauri ya Tarime mjini mkoani mara imepungua kutoka watoto 3268 mwaka 2015 hadi watoto 2628 mwaka 2017 kutokana na kuwepo na vituo vya utayari vilivyopo chini ya mpango wakuboresha elimu Nchini Tanzania(EQUIP).
Akizungumza na wandishi wa habari walio tembelea Mradi huo hivi karibuni Afisa Elimu Msingi Daniel Makorere alisema kuwa idadi ya watoto imeongezeka katika uandikishwaji kutoka watoto 9809mwaka 2015 hadi watoto 14,104 mwaka huu.
Aliongeza kuwa vituo hivyo vya utayari vilianzishwa mahususi kutokana na watoto wengi kuanza darasa la kwanza kwa kutokuwa na msingi mzuri wa elimu ya awali kutokana na shule nyingi kuwepo mbali na makazi hivyo kupelekea wazazi wengi kushindwa kuwapeleka watoto wao katika shule za awali.
“ zipo sababu nyingi zilizo pelekea kuanzishwa kwa vituo hivyo kama vile umabali wa kutoka makazi ya watu mpaka zilipo shule na kuwepo kwa vijito vingi na milima ambayo kwa watoto wadogo hawawezi kwenda shule hizo”Alisema
Kwa upande wake mratibu wa mafunzo EQUIP-TANZANIA mkoa wa mara Kiangi Elifadhi alisema mradi huu umedhaminiwa na DFID-UKAID toka Uingereza na kuwa mradi huu upo katika shule zote za msingi katika mikoa tisa ambayo ilikuwa chini kiufaulu.
Alisema mradi huu ni wa miaka sita ambapo kwa awamu ya kwanza walianza na mikoa ya Mara,Simiyu,Shinyanga,Tabora,Kigoma,Lindi na domama na kwa awamu ya pili mradi huu utafanya kazi na mikoa ya Singida na Katavi.
Aliongeza kuwa miradi hii yote inagarimu kiasi cha shilingi billion 184 ambapo kwa awamu ya kwanza uligarifu kiasi cha shilingi billion 136 na kwa mikoa miwili iliyo ongezeka itagarimu kiasi cha silingi billion 48 kwa mradi wa miaka miwili.
Elifadhi alisema kuwa wananchi wanajukumu la kuchangia katika ujenzi wa madarasa katika vituo hivyo vya utayari na inapokuwa shule shikizi basi mradi unaongezea nguvu kwa kutoa kiasi cha million 60 kwa kuongezea nguvu za ujenzi kwa kila kituo.
Kwa upande wake mratibu wa mpango wa utayari kuanza shule(SRP)Tabu Lazaro alisema kuwepo kwa vituo hivi 3 katika kijiji cha mogabiri kata ya kitare kumewezesha kwa kiasi kikubwa kwa watoto wengi kuweza kufika shule kwani vizuizi vilivyokuwepo awali vimepata ufumbuzi kwa watoto hao.
Aliongeza kuwa wazazi wamekuwa na mwamko wa kuwapeleka watoto wao katika vituo hivyo vya utayari na kuhamasika pia katika ujenzi wa vituo hivyo kwa kushindana katika mitaa yao kwani waliweza kugawana madarasa ya kujenga kwa mitaa hivyo kuweza kuhamasishana wao wenyewe.
Alisema anaishukuru serikali pamoja na mpango huu wa EQUIP-Tanzania kwa kuweza kuwafadhili kwa kuwezesha ujenzi wa vyumba vipya vya madarasa viwili,ofisi ya walimu pamoja na ujenzi wa matundu manne ya vyoo na kufanya kituo hicho cha Mtingiro kuwa na jumla ya vyumba vya madarasa saba na kuweza kuwa moja ya shule shikizi na kuweza kuanzisha darasa la kwanza kwa mwaka 2018.