Serikali kuanza kutoa chanjo ya kujikinga na saratani
Baada ya idadi ya wagonjwa wapya wa saratani kuongezeka kila siku hasa katika nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania.
Serikali
imeanza kutekeleza Mkakati wa Kitaifa wa Kuzuia na Kudhibiti Saratani
kwa kuongeza juhudi za upimaji wa dalili za saratani pamoja na kutoa
chanjo dhidi ya kirusi cha HPV kwa wasichana, ili kuondokana na tatizo
hilo.
Baada ya idadi ya wagonjwa wapya wa saratani kuongezeka kila siku hasa katika nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania.
Serikali
imeanza kutekeleza Mkakati wa Kitaifa wa Kuzuia na Kudhibiti Saratani
kwa kuongeza juhudi za upimaji wa dalili za saratani pamoja na kutoa
chanjo dhidi ya kirusi cha HPV kwa wasichana, ili kuondokana na tatizo
hilo.
Hayo
yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya
Saratani ya Ocean Road, Julius Mwaiselage na wakati akizungumza na
waandishi wa habari kuhusu Matembezi ya Hisani ya Kuhamasisha Uchunguzi
na Kuchangia Matibabu ya Saratani ya Matiti.
Amesema
takwimu zinazotolewa na Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) zinaonyesha
kuwa wagonjwa wapya milioni 14.1 hugunduliwa kila mwaka duniani.
Na
kwamba kati ya wagonjwa hao, milioni 8.2 hufariki dunia kila mwaka. Hata
hivyo amesema vifo vitokanavyo na saratani vinategemewa kuongezeka na
kufikia milioni 22 ifikapo mwaka 2030.
Mwaiselage
amesema hapa nchini, idadi ya wagonjwa wapya kila mwaka ni 44,000 na
kwamba idadi hiyo ni sawa na asilimia 12.5 ya wagonjwa wanaofika katika
Taasisi ya Ocean Road kwa ajili ya uchunguzi wa kitaalamu na matibabu.
Amesema,
asilimia 80 ya wagonjwa hao hufika hospitali wakiwa katika hatua za juu
za ugonjwa hali ambayo hupunguza uwezekano wa kupatiwa matibabu ya
kuponyesha ugonjwa.
Mwaiselage
amesema Taasisi hiyo hadi sasa imehudumia wagonjwa wa saratani 33,563
wakiwemo wagonjwa wapya na wale wa marudio 20,297.
Pia
taasisi hiyo ilifanya uchunguzi wa saratani ya matiti na shingo ya
uzazi kwa watu 7,134 ambapo watu 570 walikutwa na dalili za awali za
saratani.
Kuhusu
matembezi hayo ya hisani yanayotarajiwa kufanyika Oktoba 29, 2016,
Mwaiselage amesema lengo la matembezi hayo ni kuchangia juhudi za
serikali katika kutokomeza saratani ya matiti, kuchangia ununuzi wa
vifaa vya kutolea tiba pamoja na kuendesha zoezi la uchunguzi wa
saratani hiyo