TRA MARA WAPANDA MITI HOSPITAL YA RUFAA KUMBUKUMBU YA MWL NYERERE KWANGWA NA MARA SEC.
Mkuu wa wilaya ya Musoma Juma Chikoka amewaongoza maafisa wa mamlaka ya mapato Tanzania TRA kupanda Miti katika shule ya sekondari Mara sekondari pamoja na hospital ya Rufaa ya kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Maarufu KWANGWA katika kuelekea kilele cha maadhimisho ya miaka 30 ya malaka hiyo toka kuanzishwa Julai mosi mwaka huu.
Akizungumza katika zoezi hilo meneja wa Mamlaka hiyo mkoani Mara Masawa Masatu amesema upandaji wa miti nikurejesha uoto katika maeneo yanayoizunguka jamii hivyo mamlaka hiyo imetekeleza jukum hilo ikiwa nimkakati wa kuweka alama katikamkutimiza miaka 30 ya mamlaka hiyo.
Mkuu wa wilaya ya
Musoma Juma Chikoka amewataka wenyevti wa mitaa na watendaji kuhakikisha
wanasimamia uwekaji wa mazingira sawa katika maeneo yao ikiwemo kupanda miti
kama ilivyolekezwa na zoezi hilo litafanyika kila kaya.
“Zoezi hili linapaswa
kuwa nilasiku zote tunahitaji kuona mti kwa kila kaya tutakapopita hata
nikwenye taasisi hilo litekelezwe na kila mtu nanyie viongozi lisimamieni”Alisema
Mkuu wa wilaya ya Musoma Juma Chikoka.