WANAHABARI MWANZA NA SHINYANGA WAPEWA MAFUNZO NA TFDA.

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini TFDA imeendelea kutoa elimu kwa wadau mbalimbali kuhusu usalama, ubora, ufanisi wa vyakula, dawa, vipodozi, vifaa tiba pamoja na vitendanishi ili kusaidia kuondokana na matumizi ya dawa na vyakula vyevye madhara.

Hatua hiyo imesaidia TFDA kutekeleza vyema majukumu yake ambapo kwa mwaka 2015/17 usajili wa bidhaa umeongezeka kutoka bidhaa 7,010 hadi kufikia 9,180 hii ikiwa ni ishara njema ya kuwepo ongezeko la uelewa wa matakwa ya sheria miongoni mwa wafanyabiashara.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu TFDA, Bi.Agnes Kijo ameyasema hayo leo wakati akizungumza kwenye kikao kazi cha wahariri na waandishi wa habari kutoka mikoa ya Mwanza na Shinyanga kuhusu uhamasishaji wa sheria ya chakula, dawa na vipodozi iliyofanyika Jijini Mwanza.

Bi.Kijo amesema TFDA itaendelea kufuatilia, kuondoa na kuteketeza bidhaa ambazo hazikidhi vigenzo vya ubora, usalama na ufanisi ili kuepusha bidhaa husika kutumika ambapo amewahimiza washiriki kufikisha elimu watakayoipata kwa wananchi.

Baadhi ya wanahabari walioshiriki kikao hicho kilichofunguliwa na Mkuu wa Mkoa Mwanza John Mongella, wamesema bado kuna changamoto ya bidhaa zenye viambata sumu kuingia sokoni hivyo watatumia vyema vyombo vyao vya habari kufikisha elimu kwa jamii ili kujiepusha na matumizi ya bidhaa hizo.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu TFDA, Bi.Agnes Kijo akizungumza kwenye semina hiyo.
Mkuu wa Mkoa Mwanza akifungua semina hiyo.
Mgeni rami, viongozi wa TFDA pamoja na washiriki wakiwa kwenye picha ya pamoja.
Mgeni rasmi akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa TFDA.
Dawa bandia na duni ni hatari kwa mtumiaji.
Wanahabari na wahariri wametakiwa kutumia elimu waliyoipata kuelimisha wananchi kuhusu matumizi yasiyo sahihi ya bidhaa zenye viambata sumu.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu TFDA, Bi. Agnes Kijo (kushoto) pamoja na Naibu Mkurugenzi Idara ya Habari Maelezo, Bi.Zamarad Kawawa (kulia).
Baadhi ya washiriki kutoka mkoani Shinyanga.
                    Mshiriki kutoka Mwanza.
Wanahabari wamehimizwa kushirikiana na TFDA kutoa taarifa za uwepo wa bidhaa zenye viambata sumu.
Baadhi ya washiriki wa semina hiyo pamoja na Afisa Habari TFDA Kanda ya Ziwa (katika), Martin Malima.
                            Washiriki wa semina.
Semina hii imefanyika ukumbi wa TFDA Buzuruga Jijini Mwanza.

Powered by Blogger.