MASTA WATATU WA YANGA KUIKOSA ST.LOUIS MECHI YA MARUDIANO
WACHEZAJI 20 KUIFUATA ST. LOUIS KESHO
-Kikosi cha Yanga Sc kinatarajia kusafiri kesho asubuhi kueleka
Shelisheli tayari wa mchezo wa marejeano na wenyeji St Louis Fc kwenye
ligi ya mabingwa afrika mchezo ulipangwa kuchezwa jumatano ijayo Stade
Liete.
-Ofisa habari wa Yanga, Dismas Ten amesema jumla ya nyota 20 na
viongozi 10 kati yao 8 kutoka benchi la ufundi na 2 viongozi wa kamati
tendaji watasafiri asubuhi ya kesho kupitia Nairobi tayari kwa mchezo
wa siku ya jumatano.
"Maandalizi yote muhimu yamekwisha fanyika, timu imefanya mazoezi ya
mwisho leo tayari kwa safari hiyo, kwenye kikosi nyota waliokuwa na
majeraha ya muda mrefu kama Amissi Tambwe, Donald Ngoma, Abdallah Shaibu
na Yohana Mkomola wataendelea kukosekana hii ni kwa sababu bado
wanauguza majeraha, kucheza ugenini kuna changamoto zake lakini
tumejiandaa vizuri kwa sababu tushacheza nje mara nyingi hivyo hakuna
hofu kati yetu."
Alisema Ten
-Pia Dismas Ten amesema mchezaji Thabani Kamusoko ambaye amepona
majeraha yake hivi karibuni na kuanza mazoezi mepesi pia ameondolewa
kutoka orodha ya nyota ambao wangesafiri kueleka Shelisheli ili apate
muda wa kujifua zaidi ili kurejesha makali yake, mchezaji Obrey Chirwa
naye hayumo kwenye orodha ya wachezaji watakaosafiri kwa sababu ya
maumivu ya misuli aliyopata kwenye mchezo dhidi ya Majiamaji.
"Ilikuwa asafiri kueleka Shelisheli, lakini imelazimu benchi la ufundi
kumuondoa kwa sababu bado hajawa ‘fit’ asilimia 100, anahitaji muda wa
kujifua zaidi ili kupata utimamu wa mwili tayari kwa mapambano uwanjani,
daktari wake pia amethibitisha kuwa mchezaji anatakiwa apate muda wa
kujiweka sawa kabla hajaanza kucheza mechi kulingana na majeraha
aliyokuwa nayo".
-Orodha kamili ya wachezaji ambao watasafiri kesho kuelekea Shelishelini
kama Ifuatavyo: Makipa:- Ramadhani Kabwili, Beno Kakolanya, Youthe
Rostand. Mabeki:- Hassan Kessy, Juma Abdul, Mwinyi Haji, Gadiel Michael,
Nadir Haroub Cannavaro, Patto Ngonyani, Kelvin Yondani, na Said Juma
Makapu. Viungo:- Papy Tshishimbi, Pius Buswita, Raphael Daud, Yussuf
Mhilu, Said Mussa Bakari na Geoffrey Mwashiuya, Huku washambuliaji ni
Juma Mahadhi, Emmanuel Martin na Ibrahim Ajib