MAKALINEWS VIDEO;MSIKILIZE.PROF SOSPETER MUHONGO AAGIZA ZAHANATI YA KIJIJI CHA MWIRINGO KUANZA KUHU...

Pichani ni Mbunge wa Jimbo la Musoma vijijini Prof.Sospeter Muhongo akizungumza katika kikao katika kijiji cha mwiringo.

Sehemu ya jengo la Zahanati lilojengwa Mnamo mwaka 23-11-2011 na ilikuwa haifanyi kazi sasa kuanza kuhudumia kaya 552 katika kata ya Busambala.




Aliyevalia koti Nyeusi ni Mbunge Prof.Muhongo akisikiliza kero ya mwananchi kabla ya kuanza kikao.
******kaya 552 khudumiwa na kituo cha afya mwiringo***
Wakazi wa kijiji cha Mwiringo kata ya Busambala Halmashauri ya Musoma vijijini baada ya kuteseka kwa miaka mingi kukosa huduma ya afya katika kijiji hicho huku wa kiwa na zahanati iliyojengwa katika kijiji hicho nahaifanyi kazi sasa kero hiyo imetatuliwa na mbunge wa jimbo la musoma vijijini Prof.muhongo.
Akizungumza katika kikao na wananchi wa kijiji hicho Mbunge wa jimbo la Musoma vijijini Prof.sospeter Muhongo alimtaka Mganga Mkuu wa Halmashauri hiyo Dr.Thadeus Makwanda kuanza kutoa matibabu march 1,2018 baada ya zahati hiyo kusajiliwa rasimi.
Maamuzi hayo yalikuja baada ya Zahanati hiyo kujengwa toka mwaka 2011, ambapo nizaidi ya miaka saba huku ukosefu wa wafanya kazi pamoja na baadhi ya miundo mbinu ikiwemo meza licha ya wananchi kujitoa kujenga kituo hicho pamoja na vijana wasomi katika eneo hilo.
Mbunge huyo aliwataka wananchi kushirikiana na ofis yake ili kuhakikisha wanafanikisha adhima ya kuondoa adha ambayo wamekuwa wakiitaka kwa mda mrefu.
Pia alisema atahakikisha anakarabati zahanati hiyo nakunua thamani zinazohitajika ili wananchi wapate huduma inayotakiwa.
HABARI NA MATUKIO TUPIGIE 075295996
MENGINE ZAIDI MSIKILIZE PROFESA MUHONGO ALICHOKIZUNGUMZA.
0754295996.