FEDHA ZA MFUKO WA JIMBO MUSOMA VIJIJINI ZAANZA KUTEKELEZA MIRADI YAKE YA ELIMU.
![]() |
Nisehemu ya mafundi wakimalizia zoezi la kuezeka vyumba vya madarasa katika shule ya msingi mkapa kijiji cha kastam musoma vijijini. |
![]() |
Sehemu ya uezekaji ukiendelea. |
Na Verdiana Mgoma.Mara.
Serikari ya kijiji cha kastam imefanikiwa kutumia kikamilifu mabati yaliotokana na mfuko wa Jimbo la Musoma Vijijini chini ya Mwenyekiti wa Mbunge wa Jimbo hilo Prof. Sospeter Muhongo kwa kuezeka vyumba viwili vya madarasa na ofisi moja ya walimu.
Awali akizungumza na msaidizi wa Mbunge Ndg Verdiana Mgoma, Mwl Mkuu shule ya Msingi Mkapa David Nyakusanja ameeleza kuwa, baada ya serikari kutekeleza mpango wa elimu bure , idadi ya wanafunzi wanaojiunga na elimu ya msingi imeongezeka na kupelekea uhitaji mkubwa wa vyumba vya madarasa, Pamoja na kuwepo kwa changamoto za kitaaluma shuleni hapo adha ya vyumba vya madarasa imepewa kipaumbale baada ya wazazi wengi kuandikisha watoto wao hali hii imepelekea upungufu mkubwa wa vyumba vya madarasa.
Mwalimu huyo alisema pamoja na jitihada za ujenzi wa vyumba vya madarasa shuleni hapo lakini ongezeko la wanafunzi ni kubwa siku hadi siku na kupelekea kuwepo kwa mgawanyiko wa shule yaani A na B.
Naye Diwani wa kata ya Bukima Mh. January Simula : Ameeleza kuwa jitihada za uhamasishaji kwa kushirikiana na Ofisi ya Mbunge na umoja kutoka kwa wananchi wa kata yake umetoa mafanikio makubwa hasa baada ya kuona idara ya elimu inachangamoto nyingi.
“Kutokana na changamoto kwenye shule, tuliamua kuchukua jukumu la kubadili hali hii, lakini pia tunamshukuru sana Mbunge wetu Prof. Muhongo kwa dhamira yake kwa kushirikiana na wananchi wa kijiji cha kastam kurejesha miundo mbinu ya elimu. Hadi sasa kata yangu imefanikiwa kujenga vyumba 8 na kuezeka vyumba 7 kwa nguvu ya Mbunge wetu na kila shule imepata vitabu na madawati” alisema January
“ Inaonesha dhahiri jinsi mbunge wetu anavyopenda kuona wananchi wake wakipata elimu na kukua kimaendeleo ndiyo maana ameipa idara ya elimu kipaumbele Jimboni na kuwasii wananchi na wazazi kuwekeza kwenye elimu” Ameongeza January
Pia wananchi wa kijiji cha kastam wameipongeza serikari na Mbunge wa Musoma Vijijini kwa kuwaunga mkono kuwasaidia watoto wao kuepukana na mazingira magumu ya kujisomea
Aidha wananchi hao waliahidi kutoa ushirikiano mkubwa kwa Mbunge na serikari katika kuchangia maendeleo kwa upande wa elimu na kuwawezesha watoto wao kupata elimu iliyo bora na itakayo wasaidia katika maisha yao ya badaye.
HABARI NA MATUKIO TUPIGIE KUPITIA
0754295996.