VIDEO NA MAKALIBLOG;CHAMA CHA UZAZI NA MALEZI TANZANIA( UMATI) WATOA MAFUNZO MKOANI MARA;
Zaidi ya wasicha 30 kutoka mikoa miwili ya Tanzania wamepata mafunzo mbalimbali yaliyofanyika mkoani mara huku ya kishirikisha mikoa miwili ya tanzania bara ikiwemo mara na mwanza ikiwa lengo nikuwajengea wasichana uwezo katika nyanja mbalimbali ikiwemo haki za binadamu.
Mafunzo yaliyolenga kuwajengea uwezo wasichana katika nyanja za haki za Binadamu ukatili wa kijnsia ukeketaji stadi za maisha na uongozi ili kuwawezesha wasichana hao wazitambue haki zao na waweze kujiamini na kufanya maamuzi huru kuhusu mahusiano yao ili kupunguza mimba na ndoa za utotoni.
Mradi unatekelezwa na mashirika ya CDF katika wilaya ya tarime WADADA CENTER katika Wilaya ya ILEMELA, UMATI wilaya ya Butiama na Musoma Vijijini.
Mafunzo hayo yamefanyika katika manispaa ya Musoma mkoani Mara ambapo yameshirikisha wanafunzi zaidi ya 30 kutoka mikoa miwili ya Tanzania ikiwemo Mwanza na Mara ilikuweza kujitambua nakuweza kuwajengea katika haki za Binadamu ikiwemo ukatili wa kijinsia nakuwafanya kujiamini katika maamuzi yao wanapokuwa katika jamii.
Akizungumza katika kuhitimisha mafunzo hayo Barnabas Richard mratibu mradi amesma wanahuhakika kwa elimu ambayo wameipata wanafunzi hao itawajenga kujiamini katika kufanya maamuzi juu ya mahusiano kwa lengo la kutokomeza mimba na ndoa za utotoni.
Katika hitimisho la mafunzo hayo Mgeni Rasmi alikuwa mkaguzi toka Jeshi la kitengo cha Dawati la jinsia na watoto Bwana Lukasi Mapunda ambapo amewataka wasichana hao kutokukubali vishawishi vyovyote kwani dunia yaleo imeoza ikikumbwa na magonjwa mbalimbali.
‘’Katumieni elimu hii kuwa mabarozi kwa wenzenu kwani sasa hivi kunamagonjwa mengi ambayo nihatari semina hizi niadimu sana kuzipata ila inavotokea hizi zitumieni vizuri’’
Mafunzo hayo yametolewa na UMATI, pamoja na mashirika mengine yakijamii ikiwemo (CDF),Solution Focused Approach(WADADA CENTER) ikiwa kwa kushirikiana kwa pamoja itasaidia kupungunza hatimae kuondoa kabisamatatizo ya mimba za utotoni,ukatili wa kijinsia na manyanyaso mablimbali katika jamii zetu.
Wasichana hao wamechukuliwa wanafunzi ambao wako shuleni ikiwa nikufikisha vyema elimu ya stadi za maisha kwani kwakutumia wanafunzi hao itasaidia kuongeza mabarozi wengine kupitia shule mbalimbali zilizopo katika mradi huo kwa kutumia wasichana walioko mashuleni.
Kwa upande wake Restuta Mpate kutoka shirika la CDF yani Childrens digity Forum na Anitha Dotto Samsoni kwa WADADA CENTER wamesema kuwa watahakikisha wasichana hao wanakuwa chachu ya maendeleo katika jamii ikiwemo kuongoza mapinduzi ya ukatili kwa watoto wakike.
Kwaupande wao wasichana hao wamesema kuwa mafunzo hayo kutoka Umati yamewajenga kujiamini kuliko walivokuwa awali ambapo walikuwa wanao uwezo wakupata vishawishi mbalimbali lakini kupitia mafunzo hayo hakuna kitakacho wafanya wakudanganyika bali wao watakuwa ndio chachu ya kubadili tabia na kuwaweka katika njia iliyo sawa wasichana wengine ikiwemo kuwapa elimu waliyo ipata kutoka kwa umati.
Aidha muweshaji kiongozi kutoka Umati Bi.Jacinta Mutakyawa amesema wametumia mifano namichoro mbalimbali kuwafundisha wanafunzi hao ili lengo kuwajengea kujiamini nakuwa stadi za uongozi nautawala bora amesema kupitia elimu hiyo wasichana hao ambao sasa wako tayari kwa ajiri ya mapambano ikiwemo kuwa viongozi wa badae na wanawake wenye kujiamini.
TANGAZA NA MAKALIBLOG
TUPIGIE KUPITIA 0754295996