WANA CCM SERENGETI WATOA YA MOYONI

MWENYEKITI
wa Kijiji cha Nyamburi,kata ya Sedeko
tawi la Bisarara Wilaya ya Serengeti Mkoa wa Mara,Samsoni Matiku amekiomba
Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Mara kutoa kadi za Chama kwa wanachama ili kuepuka
matatizo mbalimbali yaliyotokea katika Uchaguzi wa mwaka Mkuu wa mwaka 2016 na
kusababisha kupoteza jimbo.
Akizungumza
katika kikao chao kilichoitishwa na Katibu wa CCM Mkoa wa Mara, Innocent
Nanzabar cha makatibu wa Chama cha Mapinduzi ( CCM) wa matawi na Jumuiya zake pamoja na Sekretaireti katika wilaya hiyo alisema kuwa kutotolewa kwa
kadi za uanachama kulisabibisha kupoteza jimbo la Serengeti jambo ambalo
liliwazunisha kwa kupoteza aliyekuwa Waziri wa Afya,Steven Kebwe ambaye kwa
sasa ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro aliyekuwa msaada kwao.
Aidha ametoa
shukrani kwa viongozi wa Chama kuwafikia kwani walikuwa wamesahaulika na kwamba
walikuwa wamesahau majukumu yao ya kuwahadhibu wanachama ambao walikuwa wanakiuka
kanuni za Chama kwa uzembe na kukiuka maadili na kusababisha Chama kuwa na
makundi ya ukabila.
Naye
Mwenyekiti wa Serikali wa Kijiji hicho, Mgendi Mniko ambaye alishuhudia
kuzaliwa kwa CCM mwaka 1977 mjini Dodoma
alisema kuwa vijana wa sasa hawatambui historia ya Chama kutokana na kutopewa katiba
na Ilani ambayo enzi ya Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere ilikuwa
kama biblia ama Msaafu na kuomba uongozi
wa Chama kugawa Ilani na katiba ya Chama ili wanachama waweze kuisoma na
kuielewa.
Akijibu hoja
zao, Katibu wa CCM Mkoa wa Mara, Innocent Nanzabar alisema kuwa kwa sasa Chama
kimetambua masuala yaliyokuwa yanasabisha wananchama wake kutojitokeza kutokana
na kuwasahau mabalozi ambao ndo walikuwa wenye Chama na kwamba Chama
kimerudishwa kwa wenye Chama.
Aliwataka kuwa
makini katika utekelezaji wa majukumu ya kazi
zao ili kuweza kupata
takwimu za wanachama zilizo sahihi kuanzia ngazi ya mashina na Matawi na kuhakikisha wanalipa ada za
Chama.
Akizungumza
katika kikao kilichofanyika katika ofisi
ya kata ya Mbalibali aliwataka mabalozi hao kuchukua fomu za kugombea nyadhifa
za juu na kufanya na kuhakikisha zoezi la uchukuaji wa fomu ngazi ya kata kwa
ajili ya maandalizi ya uchaguzi wa mwaka 2019 /2020 linafanywa vizuri bila
kificho.
Nanzabar alisema kuwa lengo la ziara yake katika Mkoa
wa Mara kati ya matawi 180 yaliyopo
ametembelea kata 80 kwa nia ya kuimarisha chama na kuwatambua
viongozi wa matawi waliochaguliwa katika uchaguzi uliomalizika hivi karibuni
na mabalozi na kutoa elimu juuu ya
muundo mpya wa uongozi uliofanyiwa marekebisho.