MAUAJI YA ASKARI KIBITI YAIBUA KAMPENI YA ‘USIUWE ASKARI WETU, MLINDE’..SIMIYU.




Mkufunzi wa usalama Barabarani wa jeshi la Polisi Mkoa wa Simiyu Kcoplo Uledi Mkumba akitoa mafunzo ya Usalama Barabarani kwa madereva wa pikipiki (Bodaboda) pamoja na madereva wa magari zaidi ya 250 kutoka katika Wilaya ya Bariadi Vijijini, mafunzo yaliyokuwa yakisimamiwa na Shirika la APEC pamoja na Jeshi la Polisi Simiyu.



Na COSTANTINE MATHIAS, Simiyu,
KUFUATIA kuwepo kwa matukio ya kutisha ya kuuawa kwa askari, pamoja na raia wengine yayoendelea katika Wilaya ya Kibiti Mkoani Pwani, taasisi ya APEC imezindua kampeini ujulikano “Usiue Askari Wetu, Mlinde”.


Taasisi hiyo ambayo siyo ya kiserikali inayojihusiha na kutoa mafunzo ya udereva kwa watu wanaoendesha vyombo vya moto, imezindua kampeini hiyo jana katika mkoa wa Simiyu.


Kampeini hiyo ilizunduliwa wakati wa kuhitimisha mafunzo kwa madereva wa pikipiki (bodaboda) madereva wa magari zaidi ya 250 kutoka katika kata za Ihuyusi, Nkololo, Gasuma, Sapiwi, Nyakabindi pamoja na Bariadi ndani ya wilaya ya Bariadi Vijijini.


Mkurugenzi wa Mtendaji wa taasisi hiyo Respicius Timanywa, alisema kuwa matukio yanayoendelea Kibiti hasa kwa kuuawa skari polisi zaidi ya 12 yameifanya taasisi hiyo kuja na kampeini hiyo.


Timanywa alieleza kuwa wamezindua kampeini hiyo ili kuhamasisha watanzania hasa wa wilaya ya Kibiti kupiga vita uhalifu huo, kutoa taarifa za wahusika, kamepini aliyoelezea kuwa itasambazwa nchi nzima.


“ Tumepoteza askari wetu wengi katika matukio haya, kila siku wanauawa watu mbalimbali pamoja na askari, na mpaka sasa hatujui nani wahusika, vyombo vya ulinzi na usalama bado vinaendelea na uchunguzi lakini bado havijafanikiwa” alisema Timanywa.


Aliongeza kuwa kampeini hiyo itapelekwa kwa madereva wa pikipiki (bodaboda) kwa kile alichobainisha vyombo vyao vya moto ndivyo vinavyotumika katika kuwasafirisha waharifu wanaotenda matukio hayo.


“ Tunataka kila mtanzania atambue kuwa huu ni uhalifu mkubwa, ni lazima tushirikiane na vyombo vya ulinzi katika kufanikisha upatikanaji wao, kuuawa askari wote hao siyo jambo dogo, hawa ni walinzi wa mali zetu lazima na sisi tuwalinde” alisema Timamwa.


Akifunga mafunzo hayo Kiamu Kaimu kamanda wa polisi Mkoa ACP Jonas Mahanga aliwataka madereva hao hasa Boda boda, kuwa makini na abiria wanaowasafirisha.
Powered by Blogger.