MAKUBWA YA IBUKA;DIWANI ,AWAONYA WANANCHI KULA MBOGA ZA MAJANI NA MATUNDA KISA KIDUDU MTU.




Wananchi wa kijiji cha Kangeme kata ya ulowa halmashauri ya ushetu mkoani Shinyanga,wametakiwa kutumia kwa uangalifu mboga za majani na matunda kutokana na taarifa za kuwepo kwa vidudu mtu anayeleta madhara kwa binadamu.
Wito huo umetolewa leo na Diwani wa kata ya ulowa PASCAL MAYENGO alipoongea na kukiri kuwepo kwa mdudu huyo katika maeneo hayo na kuwataka wananchi wa kata hiyo kuwa makini na matumizi ya mboga hizo za majani.

MAYENGO amesema wametoa taarifa za kuwepo kwa mdudu huyo katika halmashauri ya ushetu ili kuona namna utafiti wa kina unavyoweza kufanywa na wataalamu wa mimea kujua namna ya kudhibiti tatizo hilo.

Nao baadhi ya wananchi wa kijiji cha Kangeme wamesema kuwa wamemshuhudia mdudu huyo kwenye papai na kuomba wataalamu wafike kijijini hapo ili kutoa maelekezo ya kina.



Kwa upande wake mtaalamu wa Mazingira na viumbe hai EMMANUEL MAGOSO amesema chanzo cha mdudu huyo akijulikani na mara nyingi hua anatokea wakati wa jua kali na mara ya mwisho mdudu huyo alitokea mwaka 2006 na alionekana katika majani ya kisamvu pekee.
Powered by Blogger.