SERIKALI WILAYANI TARIME KUWACHUKULIA HATUA WAZAZI WANAO WAKATAA WATOTO WALIOKIMBILIA MASANGA.
Mabinti wakiwa katika Maandamano kwa baada ya kupokea Mgeni rasmi.
Mabinti wakiwa wamebeba mabango yenye ujumbe wa kupiga Vita ukatili wa kijinsia hususani Ukeketaji.
Mabango yenye ujembe mbalimbali wa kupiga vita Ukatili wa kijinsia.
Mgeni rasmi Amos Waitara ambaye ni Kaimu Afisa Elimu Msingi Halmashauri ya
Wilaya ya Tarime kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Tarime Glorious Luoga
akikata utepe katika uzinduzi wa Miaka 10 tangu kuanzishwa kwa Ushirika
wa ATFGM Masanga katika kupiga vita masuala ya Ukatili wa Kijinsia
Ukiwemo Ukeketaji, Ndoa za Utotoni, na Tohara isiyo salama kwa watoto wa
kiume.
Mgeni rasmi akifafanua jambo katika ofisi ya Ushirika wa ATFGM Masanga.
Mgeni
rasmi akikagua banda la Maonyesho kwa mabinti ambao wamesaidiwa na
Ushirika huo kwa kupewa elimu ya ujasiriamali na kuanza kushona Nguo ili
kujipatia kipatao chao.
Mgeni
rasmi akiwa katika banda la maonyesho kwa akina mama ambao walikuwa ni
Ngariba lakini baada ya kupewa Elimu juu ya madhara ya Ukeketaji sasa
wameaondokana na suala hilo na wamepewa mafunzo ya ujasiriamali na kwa
sasa wanatengeneza bidhaa mbalimbali yakiwemo Mafuta, Sabuni, Ufugaji na
Ushonaji.
Mgeni rasmi akionyeshwa mafuta yakujipaka yaliyotengeneza na wajasiriamali hao.
Mgeni
rasmi akinusa harufu ya mafuta hayo ambayo yanatengenezwa na akina mama
hao waliokuwa Ngariba kipindi cha Nyuma na sasa wameacha baada ya
kupewa Elimu na Ushirika wa ATFGM Masanga.
Sister Stella Mgaya ambaye ni Mkurugezni wa Ushirika wa ATFGM Masanga akifafanua jambo kwa mgeni rasmi.
Mwenyekiti
wa Ushirika wa ATFGM Masanga Jacob Peter akifafanua jambo katika
kufunga kambi hiyo ya wasichana na Uzinduzi wa Miaka 10 tangu kuanzishwa
kwa kambi hiyo.
Hussein Lutambi ambaye ni Afisa Mafunzo idara ya Elimu Endelevu kutoka kambuoni ya Uchimbaji wa Dhahabu Acacia North Mara.
Mariamu
Byekwaso kutoka Kampuni ya Uchimbaji wa Dhahabu ACACIA North Mara
akifafanua jambo na kupiga vita Ukatili dhidi ya Mwanamke wa Kitanzania.
Adelmarce
Emily kutoka kampuni ya Uchimbaji wa Dhahabu ACACIA North Mara
akifafanua jambo na kuomba jamii kuendelea kuthamini Mwanamke na
kuondokna na ukatili wa Kijinsia.
Sister Stella Mgaya Mkurugenzi wa Ushirika wa ATFGM Masanga.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Kambi hiyo katika Ushirika wa ATFGM Masanga.
Kutoka MKitengo cha Ustawi wa Jamii Halmashauri ya Wilaya ya Tarime Mkoani Mara.
Wasichana waliohitimu Mafunzo ya Elimu ya Tohara Mbadala na na masuala ya kupiga vita ukeketaji kwa mtoto wa kike.
Watoto wanaopatiwa Elimu ya kupiga Vita Ukatili wa Kijinsia.
Sister
Stella Mgaya Mkurugezni wa Ushirika ATFGM Masanga akifafanua jambo
katika Uzinduzi wa Miaka 10 tangu kuanzishwa kwa Ushirika huo.
Burudani.
Kati wa Ushirika wa ATFGM Masanga Dickson Joseph akisoma risala mbele ya
Mgeni rasmi ambapo amesema kuwa tangu ushirika huo kuanzishwa mwaka 2008
tayari wamepokea mabinti 2572 na kutoa Elimu kwa Ngariba na wazee wa
mila na ngariba 63 wameondokana na suala zima la Ukeketaji.
Kiapo.
Mabinti wakipatiwa vyeti vya ushiriki na Mgeni rasmi.
Mmoja wa Mabinti aliyefanyiwa ukatili na wazazi wao akieleza mkasa kwa Mgeni rasmi.
MAKALIBLOG.
Serikali wilayani tarime imesema itawachukulia hatua kali wazazi na walezi ambao wamekuwa wakiwakataa watoto wao wanaokimbia kukektwa nakukimbilia katika kituo cha kulelea wahanga hao ATFGM masanga.
Yalisemwa hayo na kaimu afisa elimu msingi halmashauri wilayani Tarime ,Bwana Amosi waitara kwaniaba ya mkuu wawilaya ya rtarime Glorius luoga wakati wakufunga kambi katika ushirika wa kutokomeza ukeketaji na ndoa za utotoni ATFGM masaga.
Waitara aliwataka masanga kuwasilisha majina ya wazazi wanaokataa watoto wao nakuwalazimisha kuolewa wanapokuwa wanahitimu mafunzo nakurudi majumbani ili serikali ichukue hatua kali zaidi yao wanaofanya hivyo.
Ambapo sasa zaidi ya mabinti 2572 wamepata mafunzo ya tohara mbadala toka mwaka 2008 hadi 2017 .