MBUNGE... PROFESA MUHONGO AKAGUA MIRADI YA MAENDELEO.....



mbunge wa jimbo la musoma Vijijini Mh; muhongo akisistiza jambo alipotembelea katika ujenzi wa kituo cha afya Bukima kushoto kwake ni Diwani kata ya BukimaJanuary Simula

Diwani kata ya Nyamradindirira Mh;Ruteli maregesi aliyesimama akizungumza katika viwanja vya shule ya msingi kasoma

Na Mkaliblog. Musoma
Mbunge wa jimbo la musoma vijijini profesa sospeter muhongo amewataka wananchi na wakazi wa jimbo hilo kuacha siasa na Badala yake waelekezo nguvu zao katika kuinua maendeleo ya jimbo lao.

Mbunge muhongo alifanya ziara yake ya siku mmoja Dec 29,jimboni kwake katika vijiji vya Bukima kilichopo kata ya Bukima,kasoma kata ya Nyamramdiririra nakijiji cha nyasaungu kata ya Ifulifu.

Lengo la kufanya ziara hiyo ilikuwa nikukagua shughuli za maendeleo ya ujenzi wa vyumba vya madarasa vinavyojengwa kwa nguvu za wananchi na fedha za mfuko wa jimbo hilo na mbunge mwenyewe.

Akiwa katika ziara hiyo profesa muhongo aliwataka wananchi wa jimbo hilo kuacha siasa zisizo na maana na badala yake waelekeze nguvu katika ujenzi wa madarasa kwani bado wanauhitaji mkubwa wa vyumba vya madarasa na mabara kwa kwajiri ya wanafunzi hivyo aliwataka kuachana kabisa na mambo hayo badala yake sasa waunge mkono jitihada zinazofanywa na viongozi wao.

Profesa muhongo amekuwa na desturi ya kuhimiza na kuchangia maendeleo huku akitilia maanani mpango wa serikali wa kila shule kuwa na maabara ambapo yeye amesisitiza pia kila shule kuwa angalau na maktaba kwa kila shule ambalo litasaidia wanafunzi kupata kujisomea nakuongeza ufanisi wao katika masomo .

Akiwa katika kijiji cha Bukima profesa muhongo alitumia nafasi hiyo kukagua ujenzi wa jengo la WARD ya mama na mtoto katika zahanati ya Bukima ambao jengo hilo liko katika hatua ya msingi.

“Aliwasisitiza watumie nguvu zao kama walivyofanya wananchi wakijiji cha nyambono ,mgango ambao kupitia nguvu zao walipokea msaada wa mifuko ya saruji kutoka wa mbunge””.alisema mbunge

Pia katika shule ya msingi kasoma Mbunge alikagua ujenzi wa vyumba vya madarasa ambapo aliwataka wanachi kuboresha miundo mbinu ili kuinua kiwango cha elimu.

Naye kwa upande wake mmoja wawananchi Bwana juma masatu maungo mkazi wa kijiji cha kasoma alimshukuru mbunge kwa kuwathamini nakuwajar wananchi wa jimbo lake kwani amekuwa ni kiongozi wa kufanya kazi nasi maneno kama wengine wanavyofanya hivyo alimtaka kutokata tamaa huku wakiahidi kumuunga mkono katika utendaji kazi wake.

“kwanza nikushukuru sana mh;kwa jitihada unazozifanya za kutuletea maendeleo kwani unajitoa kwa nguvu zako zote bila kujali itakadi yoyote”.alisema juma masatu

Aidha katika ziara hiyo Profesa muhongo aliwataka wananchi kujituma zaidi ilikufanikisha zoezi hilo nakuacha kutegemea serikali na wafadhili pekee yao.
                                             TUPE USHAURI NA MAONI YAKO HAPO CHINI                                                 MATUSI                                       (HAPANA)
                              TUPIGIE PIA KUPITIA 0754295996 KWA HABARI NA MATUKI.
Powered by Blogger.