BIASHARA UNITED MARA WATUMA SALAMU KWA ALLIANCE YA MWANZA NDUGU ZAO PAMBA WAPIGWA 2-0
MAKALIBLOG.MARA
Timu ya Biashara united mara imefanikiwa kuibuka naushindi wa mabao mawili 2 kwa bila dhidi ya timu ya pamba kutoka mwanza katika mchezo uliopigwa kunako dimba la karume mjini musoma ligi daraja la kwanza.
Timu ya Biashara United mara sasa inashika nafasi ya pili katika kundi “C”katika msimamo wa ligi kwa kuwa na pointi 20 katika kundi huku nafsi ya kwanza ikishikiliwa na Dodoma Fc kutoka Dodoma huku alliance ya mwanza ikishika nafasi ya tatu .
Kipindi cha kwanza dakika 45 zilikamilika kwa timu kwenda mapumziko bila kufungana ambapo kipindi cha pili iliwachukua dakika ya 56 Biashara kupitia kwa mchezaji Nasoro Iddi kuiandikia timu yake bao la kuongoza,na badae dakika 58 Biashara ikajipatia bao la pili kupitia kwa mchezaji Songa Gerald.
mchezo huo umechezeshwa na mwamuzi kutoka shinyanga Bwana Walter josephati kutoka shinyanga hadi dakika Tisini Biashara 2 na Pamba hawakupata kitu.
Aidha kwa uppande wake meneja wa timu ya Biashara united Amani Josiah akizungumza mara baada ya mchezo huo alisema sasa wanajielekeza katika mchezo ujao ambao watacheza na Aliance katika uwanja wakarume mjini musoma.